Ndoa ni nini?
Ndoa ni Taasisi ambayo Mungu aliianzisha kwa kusudi zima la kuweza kumfanya mwanadamu aishi kwa furaha duniani, ndo maana alipomuumba Adam akasema si vyema mtu huyu kukaa peke yake naye nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye, kumbe Mwanamke ni msaidizi wa kufanana na mwanaume.
Uhalisia wa Ndoa unakuja baada ya makubaliano ya watu wawili waliokubaliana wao wenyewe kuingia katika Taasisi hii.
Ndoa inakuwa na vitu kadhaa ili iweze kuwa ndoa imara na ya kudumu
1. Upendo
hiyo ni point muhimu sana katika kila ndoa, ili kuweza kuishi vizuri lazima kwanza mpendane ninyi kwa ninyi, kisha Upendo huo udhihirike kwa watu wengine, ndoa haiwezi kuwa ndoa njema pasipo kuwa na Upendo ulio Imara. mara nyingi watu wanaingia katika ndoa wakiwa na Matamanio na siyo Upendo wa kweli, ndo maana utaona sasa ndoa nyingi zinakufa kwa sababu ya kukosa upendo.
Mpende Mume/Mke wako kama unavyojipenda mwenyewe. Maana ndani ya Upendo kuna Uvumilivu, Utoshelevu, Kuchukuliana ninyi kwa ninyi, Hauhesabu makosa ya mwenziwe n.k.
kwa hiyo upendo una kifurushi chote cha kuweza kuidumisha ndoa yako.
Maharusi wakiwa na furaha katika siku ya Ndoa yao
MPENDE MUME/MKE WAKO KAMA UNAVYOJIPENDA MWENYEWE ILI UWEZE KUDUMISHA NDOA YAKO.
2. Mke/Mume kwanza wengine baadae:
watu wengi katika ndoa wanaingia na mizigo yao, kiasi ambacho unakuta mtu anashindwa kuendeleza ndoa yake kwa kufikiria mizigo aliyoibeba, hii pia ni pointi ya muhimu. Mfanye Mke/Mume wako kuwa kwanza kisha wengine ndio wafuatie.
Namaanisha kuwa:
tulipotoka kabla ya kuoa/kuolewa yawezekana ulikuwa na Ndugu / Rafiki yako wa karibu ambaye mlishirikiana katika mambo mengi sana, sasa unapoamua kuingia katika taasisi hii hakikisha rafiki yako wa kwanza kwa kushirikiana katika mambo mengi ni huyo Mwenzi wako baada ya kuhakikisha mizizi ya Upendo wenu imeshikamana.
Mwenzi wako ndie rafiki wako nambari moja, fikiria mtu unayelala naye ukiwa uchi, unaye share naye mambo ambayo huwezi kushare na wengine basi huyo ni zaidi ya rafiki uliyejuaana naye hata kwa kipindi cha miaka na miaka.
jenga tabia ya kumweka yeye kwanza kisha wengine baadae itakusaidia hata kuwepo na uaminifu ndani yenu, kutokuchokana kwa mapema na kila mmoja kuwa na hamu na mwenziwe.
3. Tendo la Ndoa:
kila mtu anaelewa kuwa akioa au kuolewa nini kinachowangunisha, leo nataka niwaeleze kuwa Tendo la Ndoa ni sehemu ndogo sana katika kukamilisha Ndoa lakini pia ni msingi ulio Imara kudumisha Ndoa.
tendo la ndoa ni la kulifurahia maana hapo ndipo Mungu aliporuhusu baraka ya uzao, tendo la ndoa linatakiwa kufanywa kwa bidii (Biblia inatuambia ni dhambi kufanya kazi ya Mungu kwa ulegevu) so tendo la ndoa likifanywa kwa kufurahiwa na kwa akili, bidii hakika kila mmoja nafsi yake itamfurahia mwenzi wake.
wekeni hamu/matamanio ya kukutana kwa ajili ya tendo hilo kwa kila mmoja wenu
pangeni ratiba isiyo chosha ili kuweza kukamilisha tendo la ndoa, mkifurahiana (Mungu alisema msinyimane; hapa nasema na waliooa na kuolewa) Kumbuka: ukifanya tendo la ndoa nje ya makubaliano hayo utakuwa unafanya UZINIFU na hiyo ni DHAMBI subiri wakati wako Mungu naye atakubariki kupata chaguo sahihi nawe utalifurahia.
MBARIKIWE
No comments:
Post a Comment