Wanawake tuamke jamani katika kushika fursa mbalimbali ili kuweza kujipatia maendeleo, kuna msemo ambao unasemwa sana kuwa ukimwelimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima.
Acha kubweteka mwanamke, amua leo ili kujenga msingi imara (wa uchumi) kwa ajili ya familia yako, kwanini? kwasababu kumekuwa na vilio vingi sana kwa wanawake ambao walichuma mali pamoja na waume zao kisha mwanaume anapoitelekeza familia na kuiacha mama hubaki na manung'uniko moyoni hasa mzigo wa kulea familia.
Kinachotakiwa sasa kwako mwanamke:
Anza kujijengea uwezo, fursa ya kumiliki mali yako mwenyewe.
Namaanisha nini:
katika biblia (maandiko matakatifu) Mungu anamfananisha mwanamke na merikebu ya biashara soma Mithali 31:10 - 31 (Nanukuu ule mstari wa 13 " Hutafuta sufu na kitani, hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo, afanana na merikebu ya biashara, huleta chakua chake kutoka mbali. tena huamka kabla haujaisha usiku, huwapa watu wa nyumbani mwake chakula na wajakazi wake sehemu zao)
kumbe sie mambo haya yote tunaweza kuyafanya kwa kujenga msingi imara ya uchumi ulio endelevu, nini faida ya kuwa na uchumi endelevu kwa mwanamke
1. Moyo wa mumewe humwamini, wala hatakosa kupata mapato
2. Nguvu na Hadhi ndiyo mavazi yake (maana yake ni kuwa siku zote huwa hodari, na moyo wa
ushujaa haogopi tatizo yeye hulikabili) anaucheka wakati ujao.
3. Mumewe hujulikana malangoni pa wazee:
maana yake: kila jambo utakalolifanya kwa ajili ya maendeleo ya familia yako, sifa nyingi
zitarudi kwa mume wako aliyekuoa ya kwamba amepata mke mwema. tena atajisifu kuwa
binti za watu wengi wamefanya mema lakini wewe umewapita wote
cha kufanya:
- jikubali kuwa unaweza, jipende mwenyewe
- Weka malengo yako ya muda mfupi na mrefu, kisha yaweke katika matendo
- yaamini mawazo yako kuwa yatakufikisha mahala unapopataka
- thubutu kufanya kitu cha maendeleo hata kama ni kuanzisha mradi kwa mtaji mdogo,
acha kuwa tegemezi, amka sasa mwanamke
KUMBUKA:
KINA MAMA TU JESHI KUBWA, TUNAWEZA
No comments:
Post a Comment