Kwa pamoja tunaweza

Blog hii inazungumzia masuala mbalimbali hasa changamoto mbalimbali zainazomkuta mwanamke katika harakati za kimaendeleo katika nyanja mbalimbali: iwe katika elimu, ndoa, ujasiriamali, malezi na familia.



ili kuweza kukabiliana navyo, basi blogu hii inakukaribisha wewe kwa ajili ya mchango wa mawazo ili tu kumuwezesha mwanamke wa kitanzania kufikia mafanikio na kuweza kuwa na uchumi imara na endelevu.



Nakukaribisha sana wewe kuwa mdau nambari moja wa blogu hii




KWA PAMOJA TUNAWEZA

Tuesday, August 30, 2011

Wanawake & Maendeleo: MAISHA NI FOLENI

Wanawake & Maendeleo: MAISHA NI FOLENI: MAISHA NI KAMA FOLEN AMBAYO INASOGEA POLEPOLE, HAIJALISHI MWENENDO WA FOLENI HIYO TUNACHOAMINI SIKU MOJA UTAFANIKIWA. UNACHOTAKIWA KUFANYA: ...

WANAWAKE NA UCHUMI IMARA

Wanawake tuamke jamani katika kushika fursa mbalimbali ili kuweza kujipatia maendeleo, kuna msemo ambao unasemwa sana kuwa ukimwelimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima.

Acha kubweteka mwanamke, amua leo ili kujenga msingi imara (wa uchumi) kwa ajili ya familia yako, kwanini? kwasababu kumekuwa na vilio vingi sana kwa wanawake ambao walichuma mali pamoja na waume zao kisha mwanaume anapoitelekeza familia na kuiacha mama hubaki na manung'uniko moyoni hasa mzigo wa kulea familia.

Kinachotakiwa sasa kwako mwanamke:
Anza kujijengea uwezo, fursa ya kumiliki mali yako mwenyewe. 

Namaanisha nini:
katika biblia (maandiko matakatifu) Mungu anamfananisha mwanamke na merikebu ya biashara soma Mithali 31:10 - 31 (Nanukuu ule mstari wa 13 " Hutafuta sufu na kitani, hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo, afanana na merikebu ya biashara, huleta chakua chake kutoka mbali.  tena huamka kabla haujaisha usiku, huwapa watu wa nyumbani mwake chakula na wajakazi wake sehemu zao)

kumbe sie mambo haya yote tunaweza kuyafanya kwa kujenga msingi imara ya uchumi ulio endelevu, nini faida ya kuwa na uchumi endelevu kwa mwanamke

1. Moyo wa mumewe humwamini, wala hatakosa kupata mapato

2. Nguvu na Hadhi ndiyo mavazi yake (maana yake ni kuwa siku zote huwa hodari, na moyo wa
     ushujaa haogopi tatizo yeye hulikabili) anaucheka wakati ujao.

3.  Mumewe hujulikana malangoni pa wazee: 
      maana yake:  kila jambo utakalolifanya kwa ajili ya maendeleo ya familia yako, sifa nyingi
      zitarudi kwa mume wako aliyekuoa ya kwamba amepata mke mwema.  tena atajisifu kuwa
      binti za watu wengi wamefanya mema lakini wewe umewapita wote

cha kufanya:
  • jikubali kuwa unaweza, jipende mwenyewe
  • Weka malengo yako ya muda mfupi na mrefu, kisha yaweke katika matendo
  • yaamini mawazo yako kuwa yatakufikisha mahala unapopataka
  • thubutu kufanya kitu cha maendeleo hata kama ni kuanzisha mradi kwa mtaji mdogo,
acha kuwa tegemezi, amka sasa mwanamke

KUMBUKA:

KINA MAMA TU JESHI KUBWA, TUNAWEZA

MAPUMZIKO MEMA YA EID

 All Dearz, niwatakie siku njema ya leo, pia sikukuu njema

UJUMBE WANGU KWENU:
  • Chonde chonde kwa wenye watoto kuweni waangalifu sana
  • pia msinywe pombe kupita kiasi maana ulevi ni nouma

siku ya leo iwe ya Ibada na Dua, pia mkitenda matendo mema kwa kuwakumbuka wasio jiweza kwa kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, yatima, wajane, wahitaji kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatimiza maandiko matakatifu na siku yenu itakuwa ni njema.

MBARIKIWE