Nakukaribisha sana katika Blog hii inakuhusisha wewe kushiriki nasi katika masuala mbalimbali yahusuyo Jamii, Mwanamke, Uchumi, na matukio mbalimbali yatokeayo katika Jamii yetu. Pia mada zitakazotolewa hapa, changia kila mada ili tuweze kusonga mbele kwa maoni na ushauri wako. Kwa Pamoja Tunaweza
Kwa pamoja tunaweza
Blog hii inazungumzia masuala mbalimbali hasa changamoto mbalimbali zainazomkuta mwanamke katika harakati za kimaendeleo katika nyanja mbalimbali: iwe katika elimu, ndoa, ujasiriamali, malezi na familia.
ili kuweza kukabiliana navyo, basi blogu hii inakukaribisha wewe kwa ajili ya mchango wa mawazo ili tu kumuwezesha mwanamke wa kitanzania kufikia mafanikio na kuweza kuwa na uchumi imara na endelevu.
Nakukaribisha sana wewe kuwa mdau nambari moja wa blogu hii
ili kuweza kukabiliana navyo, basi blogu hii inakukaribisha wewe kwa ajili ya mchango wa mawazo ili tu kumuwezesha mwanamke wa kitanzania kufikia mafanikio na kuweza kuwa na uchumi imara na endelevu.
Nakukaribisha sana wewe kuwa mdau nambari moja wa blogu hii
KWA PAMOJA TUNAWEZA
Friday, September 23, 2011
TUMIA UMEME MBADALA
Kama mnavyojua kwa sasa nchi yetu ina matatizo ya Mgao wa Umeme usiokwisha kila kukicha, Majenereta nayo yanapiga kelele, gharama kuyaendesha kwani yanatumia Mafuta ambayo nayo huadimika kila mara.
Sasa kuna zao jipya kutoka kwa Wazawa wa hapa hapa, Vijana wa kitanzania waliobobea katika masuala mazima na teknolojia ya kusuka Inventer (backup system) yenye uwezo wa kuendesha vifaa vya maofisini, majumbani bila tatizo, inayohimili kwa muda wa masaa 10 -12.
Huo ndo Mtambo wenyewe (hapo juu ndo Inventer, hapo Kati ni betri original za USA zinazotunza Umeme @betri ina uzito wa Kg 50)
Ni ya kudumu na kudumu na kudumu na kudumu (si chini ya miaka 15)
Watakusukia na kukuwekea kwa gharama nafuu sana.
Wasiliana nao sasa kwa namba hapo chini
+255 (0) 714 537 085
+255 (0) 765 673 575
Tatizo la kukosa umeme sasa basi maana jibu la maswali yako limepatikana sasa, wasiliana nao sasa.
KARIBU
Sunday, September 18, 2011
Wanawake & Maendeleo: NDOA
Wanawake & Maendeleo: NDOA: Ndoa ni nini? Ndoa ni Taasisi ambayo Mungu aliianzisha kwa kusudi zima la kuweza kumfanya mwanadamu aishi kwa furaha duniani, ndo maana ali...
NDOA
Ndoa ni nini?
Ndoa ni Taasisi ambayo Mungu aliianzisha kwa kusudi zima la kuweza kumfanya mwanadamu aishi kwa furaha duniani, ndo maana alipomuumba Adam akasema si vyema mtu huyu kukaa peke yake naye nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye, kumbe Mwanamke ni msaidizi wa kufanana na mwanaume.
Uhalisia wa Ndoa unakuja baada ya makubaliano ya watu wawili waliokubaliana wao wenyewe kuingia katika Taasisi hii.
Ndoa inakuwa na vitu kadhaa ili iweze kuwa ndoa imara na ya kudumu
1. Upendo
hiyo ni point muhimu sana katika kila ndoa, ili kuweza kuishi vizuri lazima kwanza mpendane ninyi kwa ninyi, kisha Upendo huo udhihirike kwa watu wengine, ndoa haiwezi kuwa ndoa njema pasipo kuwa na Upendo ulio Imara. mara nyingi watu wanaingia katika ndoa wakiwa na Matamanio na siyo Upendo wa kweli, ndo maana utaona sasa ndoa nyingi zinakufa kwa sababu ya kukosa upendo.
Mpende Mume/Mke wako kama unavyojipenda mwenyewe. Maana ndani ya Upendo kuna Uvumilivu, Utoshelevu, Kuchukuliana ninyi kwa ninyi, Hauhesabu makosa ya mwenziwe n.k.
kwa hiyo upendo una kifurushi chote cha kuweza kuidumisha ndoa yako.
Maharusi wakiwa na furaha katika siku ya Ndoa yao
MPENDE MUME/MKE WAKO KAMA UNAVYOJIPENDA MWENYEWE ILI UWEZE KUDUMISHA NDOA YAKO.
2. Mke/Mume kwanza wengine baadae:
watu wengi katika ndoa wanaingia na mizigo yao, kiasi ambacho unakuta mtu anashindwa kuendeleza ndoa yake kwa kufikiria mizigo aliyoibeba, hii pia ni pointi ya muhimu. Mfanye Mke/Mume wako kuwa kwanza kisha wengine ndio wafuatie.
Namaanisha kuwa:
tulipotoka kabla ya kuoa/kuolewa yawezekana ulikuwa na Ndugu / Rafiki yako wa karibu ambaye mlishirikiana katika mambo mengi sana, sasa unapoamua kuingia katika taasisi hii hakikisha rafiki yako wa kwanza kwa kushirikiana katika mambo mengi ni huyo Mwenzi wako baada ya kuhakikisha mizizi ya Upendo wenu imeshikamana.
Mwenzi wako ndie rafiki wako nambari moja, fikiria mtu unayelala naye ukiwa uchi, unaye share naye mambo ambayo huwezi kushare na wengine basi huyo ni zaidi ya rafiki uliyejuaana naye hata kwa kipindi cha miaka na miaka.
jenga tabia ya kumweka yeye kwanza kisha wengine baadae itakusaidia hata kuwepo na uaminifu ndani yenu, kutokuchokana kwa mapema na kila mmoja kuwa na hamu na mwenziwe.
3. Tendo la Ndoa:
kila mtu anaelewa kuwa akioa au kuolewa nini kinachowangunisha, leo nataka niwaeleze kuwa Tendo la Ndoa ni sehemu ndogo sana katika kukamilisha Ndoa lakini pia ni msingi ulio Imara kudumisha Ndoa.
tendo la ndoa ni la kulifurahia maana hapo ndipo Mungu aliporuhusu baraka ya uzao, tendo la ndoa linatakiwa kufanywa kwa bidii (Biblia inatuambia ni dhambi kufanya kazi ya Mungu kwa ulegevu) so tendo la ndoa likifanywa kwa kufurahiwa na kwa akili, bidii hakika kila mmoja nafsi yake itamfurahia mwenzi wake.
wekeni hamu/matamanio ya kukutana kwa ajili ya tendo hilo kwa kila mmoja wenu
pangeni ratiba isiyo chosha ili kuweza kukamilisha tendo la ndoa, mkifurahiana (Mungu alisema msinyimane; hapa nasema na waliooa na kuolewa) Kumbuka: ukifanya tendo la ndoa nje ya makubaliano hayo utakuwa unafanya UZINIFU na hiyo ni DHAMBI subiri wakati wako Mungu naye atakubariki kupata chaguo sahihi nawe utalifurahia.
MBARIKIWE
Tuesday, August 30, 2011
Wanawake & Maendeleo: MAISHA NI FOLENI
Wanawake & Maendeleo: MAISHA NI FOLENI: MAISHA NI KAMA FOLEN AMBAYO INASOGEA POLEPOLE, HAIJALISHI MWENENDO WA FOLENI HIYO TUNACHOAMINI SIKU MOJA UTAFANIKIWA. UNACHOTAKIWA KUFANYA: ...
WANAWAKE NA UCHUMI IMARA
Wanawake tuamke jamani katika kushika fursa mbalimbali ili kuweza kujipatia maendeleo, kuna msemo ambao unasemwa sana kuwa ukimwelimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima.
Acha kubweteka mwanamke, amua leo ili kujenga msingi imara (wa uchumi) kwa ajili ya familia yako, kwanini? kwasababu kumekuwa na vilio vingi sana kwa wanawake ambao walichuma mali pamoja na waume zao kisha mwanaume anapoitelekeza familia na kuiacha mama hubaki na manung'uniko moyoni hasa mzigo wa kulea familia.
Kinachotakiwa sasa kwako mwanamke:
Anza kujijengea uwezo, fursa ya kumiliki mali yako mwenyewe.
Namaanisha nini:
katika biblia (maandiko matakatifu) Mungu anamfananisha mwanamke na merikebu ya biashara soma Mithali 31:10 - 31 (Nanukuu ule mstari wa 13 " Hutafuta sufu na kitani, hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo, afanana na merikebu ya biashara, huleta chakua chake kutoka mbali. tena huamka kabla haujaisha usiku, huwapa watu wa nyumbani mwake chakula na wajakazi wake sehemu zao)
kumbe sie mambo haya yote tunaweza kuyafanya kwa kujenga msingi imara ya uchumi ulio endelevu, nini faida ya kuwa na uchumi endelevu kwa mwanamke
1. Moyo wa mumewe humwamini, wala hatakosa kupata mapato
2. Nguvu na Hadhi ndiyo mavazi yake (maana yake ni kuwa siku zote huwa hodari, na moyo wa
ushujaa haogopi tatizo yeye hulikabili) anaucheka wakati ujao.
3. Mumewe hujulikana malangoni pa wazee:
maana yake: kila jambo utakalolifanya kwa ajili ya maendeleo ya familia yako, sifa nyingi
zitarudi kwa mume wako aliyekuoa ya kwamba amepata mke mwema. tena atajisifu kuwa
binti za watu wengi wamefanya mema lakini wewe umewapita wote
cha kufanya:
- jikubali kuwa unaweza, jipende mwenyewe
- Weka malengo yako ya muda mfupi na mrefu, kisha yaweke katika matendo
- yaamini mawazo yako kuwa yatakufikisha mahala unapopataka
- thubutu kufanya kitu cha maendeleo hata kama ni kuanzisha mradi kwa mtaji mdogo,
acha kuwa tegemezi, amka sasa mwanamke
KUMBUKA:
KINA MAMA TU JESHI KUBWA, TUNAWEZA
MAPUMZIKO MEMA YA EID
All Dearz, niwatakie siku njema ya leo, pia sikukuu njema
UJUMBE WANGU KWENU:
- Chonde chonde kwa wenye watoto kuweni waangalifu sana
- pia msinywe pombe kupita kiasi maana ulevi ni nouma
siku ya leo iwe ya Ibada na Dua, pia mkitenda matendo mema kwa kuwakumbuka wasio jiweza kwa kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, yatima, wajane, wahitaji kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatimiza maandiko matakatifu na siku yenu itakuwa ni njema.
MBARIKIWE
Subscribe to:
Posts (Atom)
